1. OMBI LA KAZI

  • Je, nitawezaje kuomba kazi ?
    Maombi ya kazi lazima yafanywe kupitia tovuti yetu (www.ymkazi.com).
    Hata hivyo, Nakala halisi ya fomu inaweza kupokelewa na kituo cha Tathmini na Mafunzo ya Ufundi (YM- TAT Center) kwa makazi yaliyoathiriwa na Mradi wa ujenzi wa Treni ya SGR hasa kwa sehemu ambazo hazina mtandao.
    Endapo unaishi katika eneo lililoathiriwa na ujenzi wa SGR:
    Tafadhali jaza fomu ya maombi ya kazi ya Yapi Merkezi, ambayo inaweza kupatikana katika ofisi ya serikali ya mtaa iliyopo katika eneo lako.
    Tambua kwamba fomu za maombi ya kazi husambazwa na kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi kwenye serikali za mitaa pindi mradi unapohitaji nguvu kazi. (Hii inamaanisha kuwa fomu za maombi ya kazi huenda zisipatikane kwenye ofisi za serikali za mitaa katika baadhi ya nyakati).
    Kumbuka kuandika jina lako kamili kwenye fomu kama lilivyoandikwa kwenye kitambulisho chako cha NIDA.
    Pindi utakapo maliza kujaza fomu, tafadhali hakikisha unampa Mtathmini na Mafunzo ya Ufundi ili awezekufikisha kwenye Serikali yako ya mtaa.
    Tafadhali Fahamu kwamba unaweza kuomba kazi moja kwa moja kupitia tovuti (www.ymkazi.com) bila kupitia ofisi za serikali za mitaa.
  • Je, fomu za maombi ya kazi zinauzwa?
    Fomu za maombi ya kazi haziuzwi. Fomu za maombi ya kazi zilizotolewa nakala zitakataliwa, epuka kununua fomu za maombi ya kazi za uongo au zilizotolewa nakala kutoka kwa matapeli na wadanganyifu
  • Mimi ni kiongozi wa serikali ya mtaa, je, nitapataje fomu za maombi ya kazi kwa ajili ya wanakijiji wangu?
    Tafadhali andika barua rasmi ya maombi na ifikishe kwenye ofisi yoyote ya TRC, timu ya kijamii ya Yapi Merkezi, au ofisi za kituo chochote cha kazi cha Yapi Merkezi kilichopo karibu nawe. Barua yako itapelekwa kwenye kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi (YM-TAT). Wafanyakazi wa YM-TAT watawasiliana na wewe ili wakupatie fomu halisi pindi watakapopokea barua yako ya maombi kama mradi unahitaji nguvu kazi. Kama mradi hauna mahitaji ya nguvu kazi kwa kipindi hicho basi tunaomba uwashauri wanakijiji wako kutuma maombi kupitia tovuti (www.ymkazi.com) Bila kujaza fomu ya maombi ya kazi
  • Maombi kupitia tovuti (website)
    Maombi ya kazi lazima yatumwekupitia tovuti yetu (www.ymkazi.com). Tovuti hii pia ina lugha ya Kiswahili.

    Ni lazima waombaji wawe na nambari ya NIDA na nambari halali ya mawasiliano ili kutuma maombi ya kazi.

  • Je, ninaweza kufikisha ombi langu la kazi kwenye vituo vya mradi wa reli ya mwendokasi (SGR)?
    Hapana. Haiwezekani kuleta maombi moja kwa moja kwenye geti la SGR. Tafadhali zingatia jibu lililojibiwa kupitia tovuti (Pia zingatia jibu la je nijinsi gani nitaomba kazi? na majibu yanayofanana).
  • Je, ninaweza kufikisha ombi langu kwenye kituo cha uhakiki moja kwa moja YM-TAT?
    Kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi hakipokei maombi yanayoletwa na mtu binafsi moja kwa moja. Tafadhali zingatia majibu ya je ni namna gani naweza kuomba kazi? namajibu mengine yanayofanana).
  • Je, ninaweza kuomba zaidi ya nafasi moja kwa wakati mmoja?
    Hapana, unaweza kuomba kwa kazi moja tu.
  • Mimi ni mwanamke/msichana, ninaweza kuomba nafasi zipi?
    Unaweza kuomba nafasi yoyote ile.
  • Mimi ni mlemavu; je, ninaweza kuomba kazi ?
    Ndiyo, unaweza kuomba kazi yoyote ile ambayo haikuathiri kwa namna yoyote.
  • Nimefanya usaili na nimeshindwa, je, ninaweza kutuma maombi tena?
    Ndiyo, unaweza kutuma tena maombi. Lakini kutokana na idadi kubwa ya maombi ya kazi na usawa kwa kila muombaji, waombaji hawatoitwa kwa ajili ya uhakiki wa pili ndani ya mwaka huo huo, na mfumo wetu wa tovuti hauruhusu utumaji maombi mara ya pili katika mwaka.
  • Nimewahi kufanya kazi na Yapi Merkezi, je, ninaweza kutuma maombi tena?
    Ndiyo, unaweza kutuma tena maombi yako Yapi Merkezi ikiwa hukufukuzwa kwa kuvunja kanuni yoyote.
  • Je, ninaweza kubadili nafasi niliyoomba kutokana na kutokuwa na uhitaji kwenye nafasi niliyoomba?
    Huwezi kubadilisha nafasi yako ya kazi uliyoomba kwa sababu mfumo wetu wa tovuti hautakuruhusu kubadilisha nafasi ya kazi baada ya ombi lako. Unaweza kufuata tovuti yetu kwa ajili ya kujua nafasi za kazi zilizopo kisha tuma maombi ya kazi inayokufaa
  • Mimi ni dereva lakini leseni yangu imekwisha muda wake. Je, ninaweza kuomba nafasi ya udereva?
    Ndiyo, unaweza kuomba nafasi ya udereva, na unaweza kuhudhuria uhakiki. Lakini kama utafuzu, utatakiwa kuomba leseni mpya ya udereva kabla ya mchakato wa ajira.
  • Pindi ajira yangu itakapokamilika nitafanya kazi mahali nilipo sasa au nitapelekwa eneo tofauti?
    Mradi wa reli ya mwendokasi (SGR) wa Yapi Merkezi ni mradi unaohusisha eneo kubwa. Hivyo basi, kampuni inaweza kukupangia au kukuhamishia kwenye eneo lolote lile linalohusika na mradi.

2. KUITWA KWA AJILI YA UHAKIKI

  • Tayari nimeshatuma maombi, je, ni lini nitaitwa kwa ajili ya uhakiki/usaili? Tumeshatuma maombi, je, ni kwa nini hatujaitwa kwa ajili ya uhakiki/usaili?
    Ajira hutegemea juu ya uhitaji wa nguvu kazi kwenye mradi. Hivyo basi, shughuli za uhakiki na usaili hufanyika kulingana na idadi ya wafanyakazi inayohitajika kwenye mradi pamoja na nafasi za kazi zenye uhitaji. Ifahamike kuwa tunapokea maombi mengi sana ya kazi; kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi hakiwezi kushughulikia waombaji wote wa kazi kwa pamoja. Pia siyo rahisi kumpangia kila muombaji wa kazi tarehe na muda wa uhakiki/usaili.
  • Tayari nimeshatuma maombi na sijaitwa kwa ajili ya uhakiki. Je, kama bado sijaitwa ninaweza kutuma tena maombi ya kazi?
    Ajira hutegemea juu ya uhitaji wa nguvu kazi kwenye mradi. Hivyo basi, shughuli za uhakiki na usaili hufanyika kulingana na idadi ya wafanyakazi inayohitajika kwenye mradi pamoja na nafasi za kazi zenye uhitaji. Ifahamike kuwa tunapokea maombi mengi sana ya kazi; kituo cha uhakiki cha YM-TAT hakiwezi kushughulikia waombaji wote wa kazi kwa pamoja. Unaweza kuomba tena lakini kama ombi lako ya mwanzo limeshaingizwa kwenye kanzidata yetu, ombi lako la pili halitasajiliwa. Unaweza kusubiri kwa mwaka mmoja ili kutuma maombi kwa ajili ya kazi tofauti.
  • Nimepigiwa simu na kuitwa kwa ajili ya usaili. Je, nitawezaje kuthibitisha kuwa simu niliyopokea ni ya Yapi Merkezi na je, kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi kipo maeneo gani?
    Waombaji wa kazi hupewa taarifa kuhusu siku na muda wa uhakiki/usaili kwa kupigiwa simu na kutumiwa ujumbe mfupi kwenye simu. (Tafadhali tafadhali kumbuka kwamba kutoa nambari ya simu iliyosajiliwa kwa jina lako kutakulinda dhidi ya ulaghai).

    Taarifa hizi pia zitabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo nje ya jengo la YM-TAT, hivyo basi, waombaji wote wanaweza kuhakiki taarifa hizi kwa kusoma mbao za matangazo za kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi. Kituo cha uhakiki YM-TAT cha Yapi Merkezi kipo Malabi, Tabora

  • Nimepigiwa simu na kuombwa pesa kwa ajili ya kupatiwa ajira au kuharakishiwa ombi langu. Je, natakiwa kulilipia ombi langu la kazi?
    Yapi Merkezi HAISHIRIKIANI na kampuni yoyote ya kuajiri wala haina wakala yeyote yule. Yapi Merkezi haitozi kiwango chochote cha pesa kwa ajili ya maombi ya kazi, uhakiki, ajira na uharakishaji wa maombi ya kazi. Hivyo basi, tafadhali usimuamini mtu yeyote yule anayedai kutoa nafasi ya kazi au kuharakisha maombi ya kazi kwa kutoza pesa. Tafadhali KUWA MAKINI na TOA TAARIFA KUHUSU WADANGANYIFU kwa MAMLAKA HUSIKA haraka iwezekanavyo!
  • Nimeitwa kwa ajili ya uhakiki lakini sikuweza kufika kwenye muda na saa niliyopangiwa. Je, nitaitwa tena?
    Kutokana na wingi wa maombi tunatarajia waombaji kuhudhuria usaili kwa wakati kulingana na ratiba iliyopangwa. Kama hutoweza kuhudhuria ndani ya wakati, unashauriwa kutoa taarifa kwa mwakilishi wa kituo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) ili tuweze kuratibu upya usaili wako Waombaji ambao hawatoi taarifa yoyote kuhusu kutokuwepo au kuratibiwa upya wanapaswa kutarajia kwamba miadi yao inaweza isiratibiwe tena.
  • Je, mnawapatia msaada wowote wa kifedha watahiniwa mnaowaita kwa ajili ya uhakiki au usaili?
    Hatutoi msaada wowote wa kifedha kwa watahiniwa tunaowaita kwa ajili ya uhakiki au usaili. Taarifa hii hutolewa na mwakilishi wetu kwa watahiniwa wote kabla hawajaitwa kwa ajili ya uhakiki au usaili. Hivyo basi, ni chaguo la muombaji mwenyewe kuendelea na mchakato au kusitisha.

3. ENEO LA UHAKIKI

  • Kama mtu ataitwa kwa ajili ya uhakiki, je, uhakiki utafanyika Makutupora au Tabora?
    Kituo cha uhakiki kipo Tabora, hivyo basi waombaji wengi wanafanyiwa uhakiki Tabora. Hata hivyo, kwa kuzingatia eneo la kufanyia kazi, baadhi ya waombaji huenda wakafanyiwa uhakiki kwenye maeneo mengine ya mradi kama vile Itigi, Manyoni n.k.
  • Nimeitwa kwa ajili ya uhakiki lakini nimekataliwa kwenye hatua ya uthibitishaji kutokana na jina langu kuwa tofauti kwenye kitambulisho, WASIFU, na nyaraka zangu nyinginezo za maombi ya kazi. Je, nifanye nini?
    Kila muombaji anahitajika kuleta kitambulisho chake halisi na kukionesha kwa mlinzi pamoja na dawati la uthibitishaji. Muombaji yeyote ambaye kitambulisho chake kinatofautiana na WASIFU C/V wake au barua yake ya maombi na nyaraka nyinginezo atakataliwa. Muombaji ambaye ataleta kiapo cha marekebisho kutoka kwenye mamlaka husika atakubaliwa baada ya sisi kuridhishwa na kiapo chake.
  • Baada ya mtu kufanyiwa uhakiki/usaili Tabora na kufuzu/anaenda Itigi au eneo lingine ndani ya mradi ili afanyiwe uhakiki/usaili tena, na endapo atafuzu kwa nini wanamrudisha tena Tabora?
    Kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi kipo Tabora. Baadhi majaribio ya kitaalamu yanaweza kufanyika kwenye eneo la kazi lililopo karibu zaidi na muombaji, lakini waombaji watatakiwa kwenda Tabora na kufikisha nyaraka zinazohitajika wao wenyewe.

    Baadhi ya waombaji hupatwa na uoga kipindi cha uhakiki/majaribio. Waombaji wa aina hii hatuwaweki miongoni mwa walioshindwa bali huitwa kwa ajili ya kurudia uhakiki/majaribio. Ni juu ya muombaji (ambaye atapewa taarifa na mwakilishi) kuomba kurudia uhakiki/majaribio au kusitisha ombi lake.

    Baadhi ya nafasi za kazi huhitaji hatua tatu za uhakiki/majaribio na nafasi nyingi za kazi huitaji hatua za uhakiki/majaribio zisizopungua mbili, taarifa hii hutolewa na mwakilishi wetu kwa muombaji; hivyo basi, ni uamuzi wa muombaji mwenyewe kuendelea na ombi lake hadi mwisho au kusitisha.

    Muombaji anaweza kusitisha ombi lake muda wowote ule.

  • Nimefuzu uhakiki wa awali na nikaitwa kwa ajili ya uhakiki wa pili na/au wa tatu lakini nimeshindwa. Je, mnaniweka kwenye kundi la waombaji walioshindwa?
    Ndiyo, kwa bahati mbaya muombaji yeyote yule anayeshindwa hatua hizi za uhakiki huingia kwenye kundi la waombaji walioshindwa. Matokeo ya jaribio la mwisho ndiyo kigezo cha kufuzu kwa muombaji.

4. MAFUNZO KABLA AJIRA

  • Nimeitwa kwa ajili ya mafunzo, je, mafunzo haya ni ya lazima?
    Mafunzo ya kabla ya kuajiriwa ni ya lazima.
  • Nini maana ya mafunzo kabla ya ajira?
    Lengo la mafunzo ya kabla ya ajira ni kukuza ujuzi wako na kuonyesha/kuelekeza kazi inayotarajiwa kufanyika katika mradi
  • Je, mafunzo ni ya kulipia?
    Mafunzo hayalipiwi. Hutolewa bure kabisa.
  • Je, mafunzo yanachukua muda gani?
    Hutegemea na nafasi ya kazi, inaweza kuchukua kati ya siku moja hadi nne
  • Je, mnatoa usafiri, malazi, na chakula kipindi cha mafunzo?
    Hatutoi usafiri, malazi wala chakula kwa walioko kwenye mafunzo.
  • Je, baada ya mafunzo mtanipatia ajira papo hapo?
    Hapana, ajira hutegemea mahitaji ya nguvu kazi kwenye mradi. Mafunzo hayakuhakikishii kupata ajira,

5. UHAKIKI na VIGEZO VYA KUAJIRIWA

  • Je, mradi unazingatia vigezo gani pindi unapoajiri nguvukazi?
    Bila kujali nafasi ya kazi, waombaji wote lazima wafanyiwe mchakato wa usaili. Kwa vibarua (wenye ujuzi wa kati), tunazingatia sehemu ya kufanyia kazi na tunajitahidi kuajiri vibarua kutoka kwenye vijiji/maeneo ya karibu. Mahitaji ya vibarua kwenye mradi ni machache. Mradi hauwezi kuajiri kila aliyeomba nafasi ya kibarua au ya ujuzi wa kati. Uhakiki wa kitaalamu wa nafasi ya kibarua na ujuzi wa kati ni rahisi na unahusisha nyanja zifuatazo:

    • - Lazima ajue kusoma na kuandika (Kiswahili)
    • - Awe na uwezo wa kusikiliza, kuelewa, na kufuata maelekezo ya mtahini
    • - Ajue kuhesabu na mahesabu ya awali (kujumlisha, kutoa, kuzidisha, na kugawanya)
    • - Aweze kuelewa maelekezo, n.k.
  • Je, ninalazimika kujua lugha ya Kiingereza ili niweze kuomba kazi kwenye mradi wa reli ya mwendokasi (SGR)?
    Kiingereza kinahaitajika kwa nafasi kama vile uhandisi au nafasi nyinginezo za juu. Kwa nafasi za chini Kiingereza sio sharti la kuomba kazi.
  • Je, uhakiki utafanyika kwa Kiingereza pekee au utafanyika na kwa Kiswahili pia?
    Ni nafasi chache sana za kazi (hasa nafasi ya uhandisi) huitaji muombaji ajue Kiingereza. Nafasi nyinginezo za kazi hazihitaji ujuzi wowote wa lugha ya Kiingereza. Kwa sababu hii, lugha ya uhakiki hutegemea nafasi ya kazi.
  • Ni vigezo gani huzingatiwa kwa madereva? Ni kwa nini mtu mwenye uzoefu anashindwa kipindi cha uhakiki?
    Udereva ni kazi ya kitaalamu na inahitaji ujuzi wa hali ya juu wa sheria za usalama barabarani. Kampuni inahitaji kiwango maalumu cha utaalamu na uzoefu kutoka kwa madereva na waendesha mitambo ili kulinda usalama wa wafanyakazi wake na raia dhidi ya ajali mbalimbali. Hivyo basi, uhakiki wa madereva hufanyika kwa umakini wa hali ya juu sana. Madereva wengi wanashindwa uhakiki huu kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kuendesha gari, kutozingatia sheria za usalama barabarani, n.k.

6. TAARIFA JUU YA AJIRA NA UTUMAJI WA MAOMBI

  • Mara tu mtu anapofaulu kwenye usaili, atajuaje kuhusu hatua zijazo kwenye maombi yake?
    Kituo cha uhakiki cha Yapi Merkezi (YM-YM-TAT) kimeanzisha kituo cha mawasiliano ili kutoa muongozo kamili kwa waombaji. Wawakilishi wetu hutoa taarifa juu ya hatua na michakato yote ambayo muombaji anahitaji kufahamu. Unatakiwa kusikiliza kwa makini na kuelewa maelezo yanayotolewa na mwakilishi wetu.
  • Je, nitawezaje kujua ombi langu limefikia hatua gani?
    Hatutoi taarifa zozote kuhusu maombi ya kazi yalipofikia kupitia simu. Unaweza kufuatilia kwa kutuma barua pepe (email) kupitia info@ymkazi.com

    Unatakiwa uandike jina lako kama ambavyo lipo kwenye kitambulisho cha NIDA. Jina ambalo umelituma kwenye maombi yako. Email bila Majina na namba ya NIDA hazito jibiwa. Unatarajiwa kijibiwa ndani siki 45 za kazi kutokana na waombaji wengi wa kazi.

MCHAKATO WA AJIRA

  • Nimeshafanyiwa uhakiki. Je, ni lini nitaitwa kwa ajili ya michakato mingine ya ajira?
    Mchakato wa ajira unachukua muda na hatua kadhaa, hivyo basi, YM-TAT Center inafanya mchakato wa kuhakikisha utayari wa ajira. Kutegemea uhitaji wa nguvu kazi, utaalikwa wakuleta taarifa zako binafsi hivi pinde.

    Kufanyiwa uhakiki/usaili/mafunzo kwa ajili ya nafasi yoyote ya kazi haikuhakikishii kupata ajira. Waombaji wanashauriwa kurudi kwenye makazi yao na kuendelea na shughuli zao za kila siku mpaka watakapopewa taarifa zaidi kutoka YAPI MERKEZI. Watahiniwa hufahamishwa juu ya hatua hizi kabla hawajaitwa kwa ajili ya uhakiki. Ni chaguo la muombaji mwenyewe kukubali au kukataa.
  • Kwa makadirio itachukua siku ngapi hadi kupata ajira baada ya kufuzu kwenye uhakiki?
    Kwa kuzingatia mchakato wa ukusanyaji nyaraka, inakadiriwa kuchukua takribani siku 18 hadi 21 kama uongozi wa mradi utathibitisha uwepo wa mahitaji ya nguvu kazi.
  • Je, nitajuaje mchakato wangu wa ajira ulipofikia?
    Kituo cha uhakiki YM-TAT kina mwakilishi ambaye huwataarifu watahiniwa kuhusu hatua mbalimbali za maombi yao kupitia simu. Kituo cha uhakiki YM-TAT kinawashauri waombaji kutoa namba zao binafsi kwa usahihi ambazo zinapatikana muda wote ili kupokea taarifa kwa wakati.
  • Je! ni Kwanini nimekataliwa na Daktari wako kutokana na matatizo ya macho, ingawa macho yangu yapo vizuri?
    Sekta ya ujenzi inahitaji vipimo vya hali ya juu vyaki usalama. Vipimo hivyo sio tu kwa wafanya kazi bali pia kwa watu wote. Kwahio vipimo vya uono wa macho ni muhimu kwetu na kwa usalama wa mwombaji, wafanyakazi wengine, na watu wote pia, ilikuepuka ajali zinazosababishwa na matatizo ya kuona.
    Vipimo vya uwezo wa kuona ni mchakato wa uchuguzi wa awali ambayo hufanywa na Mtaalamu wa matibu wa Yapi Merkezi.
    Uchunguzi huu wa kabla ya matibabu pia unalenga kuwalinda waombaji kutokana na gharama zisizo za lazima za hati za ajira, kama vile kufungua akaunti ya benki, hati ya tabia njema ya cha polisi, usafiri, na kadhalika.
    Iwapo mwombaji atafeli kwenye vipimo vya uwezo wa kuona, Mtaalamu wa afya wa kituo cha YM – TAT anashauri kwenda kutibiwa macho na kutoa nyaraka za matibabu kabla ya kurudia uchunguzi wa macho.
    Waombaji wa kazi watakaoshindwa kwenye vipimo vya uwezo wa kuona, wanaweza kutuma maombi ya kurudia kupima baada ya kupata matibabu.
  • Inakuwaje watu kutoka maeneo mengine wameajiriwa lakini hakuna mtu hata mmoja kutoka kwenye mji wangu aliyeajiriwa?
    Yapi Merkezi hutoa kipaumbele cha ajira kwa wakazi wa vijiji/maeneo yaliyoathiriwa na mradi.

    Kwa kuongezea Yapi Merkezi haiwezi kumuajiri kila mwanakijiji kwa sababu idadi ya ajira hutegemea na mahitaji ya nguvu kazi kwenye mradi.

    YM-TAT huzingatia muhuri na sahihi kutoka ofisi za serikali za mitaa; hivyo waombaji huhesabika kuwa wanaishi maeneo ambayo wamefikisha fomu zao za maombi. Baadhi ya watendaji hupokea fomu za maombi za watokao nje ya kijiji chake. Hatuna mamlaka juu ya sahihi ya mtendaji,
  • Kwa nini wazawa wa sehemu husika hawapati kazi lakini watu kutoka maeneo mengine wanapata kazi?
    Wafanyakazi wenye ujuzi wa juu huajiriwa kutoka sehemu yoyote ndani ya Tanzania. Wafanyakazi wenye ujuzi wa kati huajiriwa kulingana na eneo la mradi linalohitaji nguvu kazi. (Tafadhali zingatia jibu na majibu yanayo fanana).
  • Kwa nini watu walioathiriwa na mradi hawapewi kipaumbele kwenye ajira?
    Project ya SGR ni kwaajili ya watanzania . kipaombele ni kwa watu walio athiriwa na sehemu ya mradi wa ujenzi (Tafadhali zingatia ,ajibu ya je ni namna gani nitaomba kazi? Ignatia namajibu mengine yanayo fanana).
  • Je, mradi unawasaidiaje vijana wa eneo husika kupata ajira?
    YM-TAT kimeanzisha nafasi za kazi za usaidizi ili vijana waweze kupata ajira kwenye mradi na kukuza ujuzi wao. Vile vile, YM-TAT kinatoa mafunzo ya muda mfupi ili kuwasaidia waombaji kukuza ujuzi wao pamoja na kujiandaa kwa ajili ya kufanya kazi kwenye mradi.
  • Je, mtu kutoka kijiji kimoja anaweza kuomba kazi ya kibarua/usafi au nafasi yoyote ya ujuzi wa kati kwenye kijiji kingine?
    YM-TAT pia inapokea maombi kupitia tovuti. Waombaji wote wanaweza kuomba bila kupitia ofisi za serikali za mitaa. Hata hivyo, kituo cha uhakiki YM-TAT huzingatia makazi ya muombaji na muombaji atatakiwa kuleta kitambulisho cha mkazi kutoka kwenye ofisi ya serikali ya mtaa kwa nafasi za kazi za ujuzi wa kati.
  • Je ninaweza kutumia kadi yangu ya bima ya afya (NHIF) kupata matibabu hospitalini wakati wa mwaliko wa matibabu?
    Ndiyo, unaweza kutumia